×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wakazi wa Katine Matungulu wahaingaika kuhusu ukosefu wa maji

Wakazi wa Katine Matungulu wahaingaika kuhusu ukosefu wa maji

Tatizo la maji kwa takriban miaka kumi kwenye kijiji cha Katine kwenye eneo la Matungulu katika Kaunti ya Machakos limewasukuma wakazi kuungana kwa pamoja kufukua Bwawa la Kwa Nzuna ambalo limekuwa tegemeo kwao lakini sasa limejaa mchanga.

Kulingana na Alice Nundu Mutiso, ukosefu wa maji umewasababishia wanawake masaibu si haba kwani wanalazimika kusafiri kilomita kadhaa kutafuta maji katika vijiji vilivyo karibu, hali ambayo huathiri jinsi wanavyoishi na familia zao.

Nundu amesema kuwa iwapo bwawa hilo litafukuliwa, basi watapata maji ya kutumia nyumbani, wapate nafasi ya kutunza maboma yao, pamoja na kufanya kilimo biashara.

"Sisi kama wanawake hatutarudi kununua mboga huko Tala, tutaipanda hapa, tuuze na tujiimarishe kiuchumi. Pia watoto wetu wa kike watakuwa salama kwa sababu hatutawatuma mbali kuchota maji."

Kauli yake Nundu imetiliwa mkazo na Joseph Kimani ambaye amesema kuwa maji ya bwawa hilo yamekuwa tegemeo kwao. Mchanga uliongia ndani ya bwawa hilo umesababisha maji hayo kukauka upesi baada ya mvua kunyesha. Aidha amesema mimea iliyokuwa ikipandwa karibu na bwawa hilo imekauka, na kwamba maji yanayotumika hasa kwa kunywa haipatikani kwani tope huingia ndani ya tanki la maji lililokuwa likitumiwa na wakazi.
" Hatuna maji safi ya kunywa na inatulazimu kununua maji mbali kwa sababu mifereji ya maji inefungika kutokana na tope.

Bwawa hili limekosa kuingia maji kufuatia mchanga mwingi, hatua ambayo imewasukuma wakazi hawa kuungana kuondoa mchanga huo.


Kulingana na Thomas Kivindyo, bwawa hilo limesababisha maafa ya mifugo na binadamu wanapoingia ndani wanakwama ndani ya tope na kufariki dunia.


"Msaada tunaohitaji kwa sasa ni kuondolewa huu mchanga lakini hata tusipopata msaada wa serikali, itatulazimu tujikaze kadri ya uwezo wetu."


Sammy Kimani Mwenyekiti wa muungano wa wakazi hao


amesema wameamua kuanzisha mradi wa kuchanga fedha ili kufukua bwawa hilo kuondoa mchanga huo, wakidai kuwa wametafuta msaada katika ofisi husika za serikali, ikiwemo ofisi ya Gavana Alfred Mutua, Mbunge wa eneo hilo Stephen Mule, Mwakilishi Wadi ya Tala Alex Kamitu, pamoja na maafisa wa Wizara ya Kitaifa ya Unyunyiziaji bila mafanikio.


"Kufikia mwezi Agosti mwaka ujao wakati wa kiangazi, tutakuwa tumeondoa mchanga huu ili msimu ujao wa mvua tupate maji na maisha yetu yarejee kama kawaida."

Share this: