×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu wengine 551 waambukizwa korona nchini Kenya

Watu wengine 551 waambukizwa korona nchini Kenya

Watu wengine 551 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya korona baada ya kupimwa kwa sampuli 4,675 katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita. Katika taarifa ya Katibu Mkuu katika Wizara ya Afya, Daktari Rashid Aman, miongoni mwa walioambukizwa, 525 ni raia wa Kenya na 26 wa mataifa ya kigeni. Wanaume walioambukizwa ni 301 huku wanawake wakiwa 250. Mtu mchanga zaidi ana umri wa miezi saba na mzee zaidi miaka 100. Kaunti ya Nairobi inaongoza kwa maambukuzi 212.

Aidha watu wengine watano wamefariki dunia na kufikisha idadi ya waliofariki kuwa elfu moja mia nne sabini na wanne. Habari njema ni kwamba watu wengine 266 wamepona ambapo mia mbili na sita walikuwa nyumbani na sitini hospitalini.

Wizara ya Afya imewataka wananchi kuzingatia mashatri mapya ya Baraza la Madhehebu mbalimbali ambalo lilitangaza kupunguza idadi ya watu wanaohudhuria harusi na mazishi. Masharti hayo yalihusu punguza idadi ya wanaohudhuria harusi hadi hamsini huku jamaa wa karibu pekee wakiruhusiwa kula wakati wa harusi huku wanaohudhuria mazishi wakiwa 100 japo kumi na watano pekee ndio watakaoruhusiwa katika kaburi wakati wa mazishi.

Wakati uo huo, Kenya imepiga hatua kubwa katika kukabili maambukizi ya virusi vya HIV ambapo visa takriban elfu thelathini na sita viliripotiwa mwaka 2018 kulinganisha na mwaka wa 2012 ambapo vilikuwa elfu mia moja na sita. Aman hata hivyo amesema idadi ya watu waliopomwa virusi hivyo ilipungua kati ya mwezi Machi na Aprili na Juni mwaka huu huku kipindi cha baina ya Juni na Julai upimaji huo ukipungua kwa asilimia 33.