×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kalonzo awataka Wakenya kujiepusha na siasa za mgawanyiko

Kalonzo awataka Wakenya kujiepusha na siasa za mgawanyiko

Kinara wa Wiper, Kalonzo Musyoka amewashauri Wakenya kukomesha siasa za migawanyiko wakati wa kuzungumzia Mswada wa Marekebisho ya Katiba wa mwaka wa 2020.

Musyoka amesema marekebisho ya katiba hayalenga kuonesha ubabe wa kisiasa baina ya Kinara wa ODM Raila Odinga na Naibu wa Rais William Ruto.

Aidha anashikiniza kukamilishwa mara moja kwa shughuli ya kutia saini mswada huo kabla ya kudhibitishwa na Tume ya Uchaguzi, IEBC ili kufanikisha kufanyika kwa kura ya maamuzi.

Musyoka amezungumza leo hii katika ofisi za Kamati ya Kiufundi ya BBI, ambapo aliwaongoza wabunge wa Wiper kutia saini mswada huo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kiufundi ya BBI, Dennis Waweru amesema kwamba huenda kamati hiyo ikakusanya zaidi ya saini milioni tano kulinganishwa na moja zinazohitajika.