
Naibu wa Rais William Ruto amesema hapingi mchakato wa marekebisho ya katiba ila anachohimiza ni kuhakikisha kwamba hakuna ushindani wakati wa kura ya maamuzi.
Akizungumza wakati wa hafla ya mazishi ya mamaye Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri, Elizabeth Wanjiru, Ruto amesisitiza kwamba kuna anayepinga mswada wa marekebisho ya katiba.
Aidha amekiri kwamba pia yeye na Rais Kenyatta walikuwa na tofauti zao ila wakaamua kujadiliana kwa manufaa ya taifa hatua ambayo inapaswa kuingwa katika mchakato wa kuifanyia katiba marekebisho.
Wakati uo huo Ruto ameikosoa Idara ya Upelelezi DCI kwa kuzifungua upya faili za kesi za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007, akisema hatua hiyo inaibua ukabila.
Awali Mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua ameendelea kumshambuli Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Upelelezi DCI George Kinoti kufuatia madai ya kuzifungua upya faili za kesi za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.