×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mahakama yasitisha kwa muda hoja ya kumbandua Gavana Sonko

Mahakama yasitisha kwa muda hoja ya kumbandua Gavana Sonko

Gavana wa Nairobi, Mike Sonko amepata afueni ya muda baada ya mahakama kusitisha mpango wa Bunge la Kaunti ya Nairobi kujadili hoja ya kumbandua mamlakani.

Jaji Nzioka Makau ametoa agizo hilo ili kutoa muda wa kusikilizwa kwa kesi iliyowasilishwa na Sonko kupinga kujadiliwa kwa hoja hiyo.

Katika agizo hilo Jaji Makau amemtaka Spika wa Nairobi vilevile wa Seneti kutoandaa kikao chochote kujadili hoja yoyote inayohusiana na hatma ya Sonko.

Mwakilishi wa Wadi ya Kileleshwa Micheal Ogada ambaye vilevile ndiye Kinara wa Wengi katika bunge hilo aliwasilisha hoja hiyo bungeni kwa misingi ya kesi za ufisaidi vilevile matumizi ya mabaya ya ofisini.

Katika hoja hiyo Ogada anadai kwamba Sonko amekuwa mahakamani mara si moja akihusishwa na sakata mbalimbali za ufisadi na kwamba hafai kuendelea kuhudumu kama Gavana.

Agizo la mahakama linajiri siku moja baada ya Gavana Sonko kuzuiliwa kwa muda na maafisa wa polisi waliowatawanya wawakilishi wadi wanaoegemea upande wa Sonko walipokuwa wakitaka kuwahutubia wanahabari kuhusu msimamo wao katika mchakato wa kumbanua Sonko mamlakani.