
Madaktari wamerejelea kauli yao ya awali kwamba kamwe hawatarejea kazini baada ya mgomo wao kung'oa nanga tarehe 7 mwezi huu hadi pale serikali itakapotekeleza matakwa yao kikamilifu.
Akiwahutubia wanahabari muda mfupi uliopita, Chibandi Mwachonda ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Madaktari, KMPDU ameapa kutotishwa na vitisho kutoka kwa baadhi ya taasisi serikalini akisisitiza kwamba sharti matakwa ya madaktari yashughulikiwe.
Miongoni mwa masuala ambayo wanataka yazingatiwe wahudumu wa afya kupewa vifaa vya kujikinga kutokana na virusi vya korona, kulipw amarupurupu pamoja na kuongezwa kwa idadi ya madaktari nchini.