×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wagonjwa wengine 17 wa Covid-19 wafariki dunia, 72 wakilazwa ICU

Wagonjwa wengine 17 wa Covid-19 wafariki dunia, 72 wakilazwa ICU

Watu wengine mia tatu na wawili wameambukizwa virusi vya korona baada ya sampuli elfu tatu na thelathini na nane kupimwa katika saa ishirini na nne zilizopita.

Maambukizi haya ni sawa na asilimia tisa nukta tisa kulinganishwa na jana ambapo ilikuwa asilimia kumi nukta sita sita. Kufikia sasa jumla watu elfu themanini na watatu mia sita kumi na wanane wameambukizwa korona nchini.

Kaunti ya Nairobi inaendelea kuongoza kwa maambukizi leo hii ikiwa na mia moja thelathini na wanne, Kisumu ishirini na sita, Kitui, Marsabit na Nyeri kumi na sita kila kaunti. Aidha maambukizi kwenye kaunti ya Mombasa yameanza kupungua baada ya kurekodi kumi na watatu sawa na Meru na Machakos, Nakuru na Kiambu tisa, Uasin Gishu wanane, Embu na Busia wawili.

Kilifi, Laikipia , Murang'a, Kakamega, Makueni, Samburu, Tana River na Kericho zimerekodi mgonjwa mmoja kila kaunti. Katika maambukizi hayo watu mia mbili themanini na sita ni Wakenya huku kumi na sita wakiwa raia wa kigeni.

.Wagonjwa wengine mia tatu tisini na tisa wamepona ambapo mia mbili themanini na saba walikuwa wakihudumiwa nyumbani huku themanini na wawili wakiwa kwenye hospitali mbalimbali. Kwa jumla waliopona ni elfu hamsini na tano, mia tatu arubaini na wanne.

Katika taarifa, Wizara ya Afya aidha imesema wagonjwa wengine elfu moja mia mbili themanini na wawili wamelazwa kwenye hospitali mbalimbali, wengine elfu nane mia nne na watano wakihudumiwa nyumbani.

Wakati uo huo wagonjwa wengine 72 wamelazwa ICU, 47 wakiwekewa vipumuzi, 92 wakiwekezwa oxijeni na 20 wakihitaji uangalizi wa karibu.

Hata hivyo wagonjwa wengine kumi na saba wamefariki na kufikisha elfu moja mia nne sitini na tisa walioaga dunia kutokana na makali ya Covid-19.