×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed akana taarifa kuwa kikosi cha serikali kimewaua raia katika eneo laTigray

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed akana taarifa kuwa kikosi cha serikali kimewaua raia katika eneo laTigray

Waziri Mkuu wa Ethiopia  Abiy Ahmed amekana taarifa kwamba kikosi cha serikali kimewaua raia katika eneo la Tigray.

Abiy amewaambia Wabunge mapema leo kwamba hakuna raia hata mmoja ameuliwa kufuatia mapigano yanayoendelea.

Abiy aidha amesema kikosi hicho hakitaharibu Mekelle, mji mkuu wa Tigray, baada ya kutwaa mji huo hapo jana.

Hadi sasa hakuna taarifa kamili kutoka kwa wanachama wa People’s Liberation Front TPLF, ambao wanaishtumu serikali kwa kuwalenga raia kutumia makombora.

Hapa jana, kiongozi wa TPLF alisema kwamba serikali ya Ethiopia ilikuwa imeanza kuwateka nyara raia katika eneo la Mekelle.