
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia Joe Mucheru amewahakikishia Wakenya kuwa data zote zinazowasilishwa mtandaoni wakati wa kutia saini kuidhinisha ripoti ya BBI zitalindwa ili kutotumiwa visivyo.
Akizungumza kwenye Kaunti ya Nyeri baada ya kutia saini yake kuidhinisha ripoti hiyo, Waziri Mucheru vilevile ameeleza kuwa Tume huru ya Uchaguzi na mipaka IEBC itahakikisha kuwa kuna uwazi wakati wa kuweka saini mtandaoni na kwenye vitabu
Kwa upande wake, Seneta wa Nyeri Ephraim Maina amekariri kuwa kaunti hiyo itaendelea kusisitiza kuongezwa kwa eneo bunge moja zaidi hata baada ya kufanyika kwa kura ya maamuzi.