×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Ubabe wa uongozi katika Chama cha Ford Kenya wazidi kutokota

Ubabe wa uongozi katika Chama cha Ford Kenya wazidi kutokota

Huenda mgogoro wa uongozi katika Chama cha Ford Kenya ukachukua mkondo mpya baada ya Mwenyekiti wa chama hicho katika Kaunti ya Kisii Job Nyakenyanya kubanduliwa uongozini.

Nyakenyanya ametimuliwa kufuatia msimamo wake wa kuunga mkono azma ya Mbunge wa Kanduyi Wafula Wamunyinyi ya kutaka kumbandua uongozi Kinara wao Moses Wetangula.

Kinara wa Chama hicho Moses Wetangula aidha amemteua Timothy Arege kuwa mwenyekiti wa Ford Kenya katika Kaunti ya Kisii kikaimu hadi pale uchaguzi wa chama utakapofanyika.

Wetangula aidha amewasuta Wamunyinyi na Katibu wa Ford Kenya Eseli Simiyu kwa kupanga njama ya kumbandua uongozini.

Mabadiliko ya uongozi katika Chama cha Ford Kenya yanajiri mwezi mmoja tu baada ya Wamunyinyi anayepinga uongozi wa Wetangula kukwepa mtengo wa polisi katika mkahawa mmoja alipokuwa akiwahutubia wanachama kwenye kaunti hiyo kuhusu jinsi ya kumbandua Wetangula.

Aidha yanajiri siku kadhaa tu baada ya Wamunyinyi na washirika wake kuahirisha mkutano wa wanachama wa Ford Kenya uliopangwa kufayika katika ukumbi wa Bomas wa kutaka kumbandua Wetangula katika nafasi ya kinara wa chama hicho.