×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 7 wafariki dunia kutokana na Covid-19, 711 wakiambukizwa korona

Watu 7 wafariki dunia kutokana na Covid-19, 711 wakiambukizwa korona

Watu wengine 711 wameambukizwa virusi vya korona baada ya kupimwa kwa sampuli elfu sita mia sita sabini na mbili katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita.

Maambukizi ya leo ni sawa na asilimia 10.66. Katika maambukizi hayo watu mia sita tsini na wawili Wakenya huku kumi na tisa wakiwa raia wa kigeni. Aidha mtoto wa mwaka mmoja ni miongoni mwa walioambukizwa virusi hivyo hatari na mzee zaidi akiwa wa umri wa miaka tisini na miwili. Kwa jumla walioambukizwa nchini ni elfu themanini na watatu, mia tatu kumi na sita.

Katika takwimu hizo, Kaunti ya Nairobi imeendelea kuongoza kwa kuwa na 190, Mombasa 88, Nakuru 78, Nyandarua 35, Murung'a 34, Kitui 30, Machakos 28, Nyeri 27, Embu 25, Busia 21, Kiambu 17, Vihiga 16, Kisumu 13, Kilifi 11, Isiolo 11, Meru 10, Turkana 10, Kirinyaga na Bungoma 9 kila kaunti, Laikipia 8, Kakamega 7, Kajiado 6, Kwale na Homabay 5, Makueni 4, Kisii, Uasin Gishu na Migiri kila kaunti na Nandi, Tharaka-Nithi, Samburu, Baringo, Kericho, Taita Taveta, Lamu na Bomet 1 kila kaunti.

Aidha wagonjwa wengine mia tano sabini na sita wamepona Covid-19 ambapo mia nne sitini na sita walikuwa wakihudumiwa nyumbani na wengine mia moja na saba kwenye hospitali mbalimbali. Kwa jumla waliopona kufikia sasa ni elfu hamsini na nne, mia tisini sabini na watano.

Wakati uo huo elfu moja mia mbili sitini na wawili wamelazwa kwenye hospitali mbalimbali na wengine elfu saba mia nane na sita wakihudumiwa wakiwa nyumbani. Wagonjwa wengine sitini na wanane wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa Mahututi ICU, arubaini na wawili wakiwekewa vipumuzi, tisini na sita wakitumia oxijeni huku ishirini na watatu wakihitaji uangalizi wa karibu.

Hata hivyo saba zaidi wamefariki kutokana na makali ya Covid-19 na kufikisha jumla ya walioaga kuwa elfu moja mia nne hamsini na wawili.