×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Vita vya ubabe wa kisiasa waibuka tena baina ya Gavana Joho na Mvurya

Vita vya ubabe wa kisiasa waibuka tena baina ya Gavana Joho na Mvurya

Vita vya ubabe wa kisiasa vimeibuka tena baina ya Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho na wa Kwale Salim Mvurya kufuatia uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Eneo la Msambweni.

Gavana Joho ambaye ni Naibu Kinara wa ODM amekuwa akiendeleza kampeni za mgombea wao Omar Boga huku Mvurya akiongoza kampeni za mgombea huru anayeungwa mkono na Naibu wa Rais William Ruto, Faisal Abadallah Bader.

Kwenye misururu ya kampeni zake, Mvurya amekuwa akimlaumu Joho kwa kwa kukita kambi kwenye eneo la Msambaweni na kuendeleza kampeni kwa ajili ya Boga ambaye wamekuwa wakimtaja kuwa chaguo la serikali. Mvurya amewataka wakazi kupuuza wito wa Gavana Joho na kumchangua Faisal kuwa mbunge wao.

Kwa upande wake Gavana Joho amesisitiza kwamba Boga ndiye mgombea anayependekezwa na serikali kauli ambayo imesisitizwa na Seneta wa Kwale Issa Juma Boy akisema Gavana Joho ana haki ya kutembea eneo lolote nchini kumfanyia kampeni mgombea wa ODM kwa kuwa ndiye Naibu Kinara.

Aidha akizungumza wakati wa kampeni hizo, Boga ameahidi kuhakikisha kwamba masuala ya uchumi katika eneo la Msambweni vilevile Pwani kwa jumla yanafanywa kipaumbele katika miradi ya serikali. 

Licha ya Chama cha Jubilee kukosa kuwa na mgombea wake katika uchaguzi huo, Naibu wa Rais William Ruto alitangaza kumuunga mkono Faisal na hata mara si moja wandani wake wakiwamo waliokuwa maseneta Hassan Omar wa Mombasa, Johnston Muthama wa Machakos, Bony Khalwale wa Kakamega wamekuwa wakiendeleza kamepeni katika eneo la Msambweni kwa ajili ya Faisal.

Mapema mwezi huu viongozi wa Chama cha ODM katika eneo la Pwani wakiongozwa na Gavana Joho walikita kambi katika eneo hilo na kufanya kampeni za nyumba kwa nyumbani kuwarai wakazi kumchagua Boga ili kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Suleiman Dori aliyefariki mapema mwaka huu.

Uchaguzi huo utafanyika tarehe kumi na tano Mwezi Disemba mwaka huu.