
Viongozi wa Kaunti ya Laikipia wameendelea kuipigia debe ripoti ya mwisho ya Mpango wa Upatanishi BBI wakisisitiza kwamba itatatua changamoto zinazowakumba Wakenya.
Wakiongozwa na Gavana Nderitu Muriithi viongozi hao wametaja suala la kuongezwa kwa mgao wa fedha kwenye kaunti na kutengwa kwa Hazina ya Fedha za Maendeleo ya Wadi kutahakikisha maendeleo mashinani vilevile kwa kuongezwa eneo bunge moja.
Amewataka wakazi kuwa tayari kutia saini mswada wa marekebisho ya katiba wa mwaka 2020 ili kufanikisha kuwapo kwa kura ya maamuzi.
Wakati uo huo Mwakilishi Wadi Maalum katika Bunge la Kaunti hiyo Irene Wacuka amesema kuongezwa kwa maeneo bunge kwenye kaunti hiyo kutaboresha huduma mashinani kwa kuwa kaunti hiyo itapata wadi nyingine.
Kwa upande wake Spika wa Bunge la Nyandarua Ndegwa Wahome ambaye vilevile ni Mwenyekiti wa Baraza la Mabunge ya Kaunti amesema baraza hilo litatoa mwelekeo wake hivi karibuni kuhusu BBI.