×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Nina jukumu la kikatiba kumsaidia Rais -Ruto

Nina jukumu la kikatiba kumsaidia Rais -Ruto

Nina jukumu la kikatiba kumsaidia Rais.

Ndiyo kauli ya Naibu wa Rais William Ruto.

Katika Mtandao wa Twitter, Ruto amesema kwa sasa mapendekezo tata ya BBI yamerekebishwa na kwamba lengo kuu kwa sasa ni kutafuta mwafaka wa kuzuia ushindani mkali wa kisiasa wakati wa kura ya maamuzi.

Ruto ambaye amepuuza madai kwamba amebadili msimamo kuhusu BBI, amekariri kwamba haja yake kuu ilikuwa kuhakikisha kila mmoja ananufaika, na kwamba hakuna hali ya kuwagawanya wananchi katika makundi mawili hasimu.

Amesema nikimnukuu,

I've CONSTITUTIONAL duty to assist my boss,the PRESIDENT.We've made IMPROVEMENTS to BBI post bomas. Now working on CONSENSUS for kenyans to have REAL CHOICES to decide/vote while avoiding yes/no,all/nothing DIVISION.We avoided lose-lose we can overcome win-lose to achieve WIN-WIN. Mwisho wa Nukuu.

Hata hivyo, Mbunge wa Suna Mashariki Junet Muhammed ambaye pia ni mmoja wa Wenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya BBI, amemjibu Ruto akimtaka atie saini ya kufanikisha kura ya maamuzi jinsi Rais alivyofanya.

Junet amesema nikimnukuu,

Boss the signature collection is on... when are you signing since your boss the PRESIDENT signed on Wednesday Story zingine ya yes/no and yes/yes baadaye, Mwisho wa Nukuu.

Wakati uo huo, Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen ameshangazwa na unafiki wa chama cha ODM akisema hafahamu ni kwa nini washirika wa Raila Odinga wanashinikiza Ruto apinge BBI hata baada ya kurekebisha baadhi ya mapendekezo jinsi Ruto alivyotaka.

Jana katika mtandao wa Twitter, Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Ofisi ya Naibu wa Rais Emmanuel Tallam aliashiria kwamba huenda mrengo wa Ruto ukakosa kushiriki katika kampeni ya kupinga BBI jinsi ilivyotarajiwa, na kwamba ushindani mkali wa kisiasa utarajiwe tu wakati wa kampeni za mwaka wa 2022.

Awali, Kauli ya Ruto katika mtandao huo wa Twitter ilitafsiriwa na wengi kuwa tangazo la kuonesha amebadili msimamo japo bado hajatangaza rasmi endapo ataunga kura ya maamuzi au la.