×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Polisi aliyemuua kijana wa miaka 20 Busia, kuzuiliwa hadi Jumatatu

Polisi aliyemuua kijana wa miaka 20 Busia, kuzuiliwa hadi Jumatatu

Afisa wa Polisi anayedaiwa kumuua kijana mwenye umri wa miaka 20 katika eneo la Malaba kwenye Kaunti ya Busia kwa madai ya kutovaa maski, atazuiliwa korokoroni hadi Jumatatu atakapofikishwa mahakamani.

Kukamatwa kwa afisa huyo kumejiri baada ya wakazi wa Malaba kuandamana hadi katika Kituo cha Polisi cha Malaba, wakikashifu kitendo cha polisi huyo kumuua kijana huyo kwa jina Ezekiel Odera, ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Upili ya Kolanya katika kaunti ya Busia.

Majira ya jioni wakazi wa Malaba waliandamana kwa mara ya pili wakilalamikia kuuliwa kwa mwanafunzi huyo.

Kwa mujibu wa wakazi hao, polisi wamekuwa wakitumia nguvu kupita kiasi wakati wa kutekeleza masharti ya kukabili Korona.

Awali waliandamana wakishinikiza maafisa wote wa Kituo cha Polisi cha Malaba, kuhamishwa kwa madai kwamba wamekuwa wakiwahangaisha kwa kuwanasa na kuwalazimisha kutoa hongo.

Tayari familia ya kijana aliyeuliwa inataka serikali kuingilia kati na kuhakikisha inapata haki na fidia.

Wazazi wa marehemu ambaye alipigwa risasi na afisa mmoja wa polisi katika eneo la Malaba, wamewalaumu polisi kwa kujichukulia sheria mikononi hivyo kutaka serikali kuingilia kati.

Mama wa marehemu amesema maafisa wa polisi hawakushughulikia matibabu ya mwanao licha ya mmoja wao kumjeruhi kwa risasi.

Viongozi wa kaunti ya Busia wakiongozwa na Gavana Sospeter Ojaamong wamekashifu kitendo hicho wakiwataka polisi kukoma kuwahangaisha wananchi.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi katika kaunti ya Busia John Nyoike amewataka wakazi wa kaunti hiyo kudumisha amani akiahidi kwamba sheria itafuatwa ili kuhakikisha familia inapata haki.