×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

949 waeambukizwa korona, 4 wakiaga dunia

949 waeambukizwa korona, 4 wakiaga dunia

Watu mia tisa arubaini na tisa wameambukizwa korona katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita.

Idadi hii imetokana na sampuli elfu nane, mia tatu kumi na moja zilizopimwa katika kipindi hicho, kumaanisha viwango vya maambukizi leo ni asilimia 11. 4 ilikinganishwa na asilimia 16. 5  ya jana.

Jumla ya watu walioambukizwa korona nchini sasa ni elfu thelamini na mbili, mia sita na watano.

Miongoni mwa waliotangazwa leo kuambukizwa, wote ni wakenya wasipokuwa thelathini na sita ambao ni raia wa kigeni.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema Kaunti ya Nairobi imerekodi idadi ya juu zaidi ambayo ni watu mia nne, mia moja thelathini na wanane Kiambu, Mombasa sabini na mmoja, Kakamega arubaini na tisa, Kericho thelathini na watatu, Kisii thelathini, Nyamira ishirini na sita, Machakos ishirini na wanne na Kisumu kumi na wanane.

Watu wengine mia mbili  sabini na wanne wamepona na kufikisha idadai jumla kuwa elfu hamsini na wanne mia tatu tisini na tisa. Mia mbili ishirini na wanne miongoni mwao walikuwa wakihudumiwa nyumbani na hamsini walikuwa kwenye hospitali mbalimbali.

Watu wengine wanne wamefariki dunia na kufikisha jumla kuwa eldu moja mia nne arubaini na watano.

Kuna wagonjwa elfu moja mia mbili arubaini na wanne wa COVID-19 waliolazwa kwenye hospitali mbalimbali huku wengine elfu saba  mia nane ishirini na tisa wakiendelea kuhudumiwa wakiwa nyumbani. Walio ICU ni wagonjwa hamsini.