
Polisi wanawazuilia vijana kumi na wanane waliokatwa mtaani Kahawa Sukari kwenye Kaunti ya Kiambu wakisherehekea.
Inaarifiwa kumi na wanane hao ni wa kati ya umri wa miaka kumi na sita na kumi na minane, waliokuwa wakisherehekea siku ya kuzaliwa kwa mmoja wao wakinywa pombe.
Mkuu wa Polisi wa Ruiru Geoffrey Githinji amesema walikamatwa kwa kukiuka masharti ya kuzia maambukizi ya virusi vya korona.
Amewashauri wazazi kuhakikisha wanafahamu waliko wanao huku akisema wataachiliwa baadaye leo.
Katika siku za hivi karibuni polisi wamekuwa wakiwakamata vijana wanaopatikana kwenye sherehe wengi wakiwa wanafunzi wa shule za msingi na upili.
Wiki jana polisi waliwatia mbaroni wanafunzi arubaini na wanne waliokuwa kwenye sherehe katika mtaa wa Mountain View jijini Nairobi. Walipatikana na pombe na bangi.