×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Polisi wampiga risasi mwanaume kwa kutovaa maski, Busia

Polisi wampiga risasi mwanaume kwa kutovaa maski, Busia

Familia ya kijana aliyeuliwa na polisi kwa kupigwa risasi katika kaunti ya Busia kwa madai ya kutovaa maski sasa inataka serikali kuingilia kati na kuhakikisha inapata haki.

Wazazi wa marehemu ambaye alipigwa risasi na afisa mmoja wa polisi katika eneo la Malaba alipokuwa akikamatwa kwa kutovaa maski, wamewalaumu maafisa wa polisi kwa kujichukulia sheria mikononi hivyo kutaka kufidiwa.

Mama wa marehemu amesema maafisa wa polisi hawakushiriki katika juhudi za kuhakikisha anapata matibabu hata baada ya kumjeruhi kwa risasi.

Gavana wa Busia Sospeter Ojamomong amekashifu kitendo hicho akiwataka maafisa wa polisi kuzingatia sheria baada ya kuwaua wananchi.

Haya yanajiri muda mfupi tu baada ya wakazi wa Malaba kwenye Kaunti hiyo ya Busia kuandamana wakikashifu kisa hicho cha afisa wa polisi kumuua mwananchi kwa sababu ya kutekeleza masharti ya kudhibiti Korona.

Wakazi hao wamewalaumu maafisa wa Kituo cha Polisi cha Malaba kwa madai ya kuwahangaisha kila mara kwa kuwanasa na kuwalazimisha kutoa hongo kwa kisingizio cha kukiuka masharti ya Korona.

Kwa sasa wakazi hao wanashinikiza kuhamishwa kwa maafisa hao wa polisi, wakisema wamekuwa kero baada ya kutumia masharti ya Korona kuwa kitega uchumi.

Kufuatia kisa hicho, waandamanaji hao wameamua kukiuka uvaaji maski ambapo anayetikana nayo anachapwa huku wakitatiza shughuli za uchukuzi katika barabara zote kwenye eneo la Malaba..

Kijana aliyeuliwa kwa kupigwa risasi na polisi kwa sababu ya kutovaa maski, ni mwenye umri wa kati ya miaka 27 na 30.

Inaarifiwa kwamba mwanamume huyo alikiuka agizo la polisi waliokuwa wameweka kizuizi cha barabarani katika eneo la Malaba hali iliyomfanya mmoja wao kumfyetulia risasi.