×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mvua kubwa kunysha nchini wikendi hii

Mvua kubwa kunysha nchini wikendi hii

Mvua kubwa imeshuhudiwa kwenye maeneo mbalimbali nchini usiku wa kuamkia leo ikiwamo jijini Nairobi huku Idara ya Utabiri wa Hali ya Anga ikisema kwamba mvua hiyo itaendelea wikendi hii na kupungua katika kipindi cha siku tatu zijazo. Hata hivyo mvua kubwa itanyesha kwenye kaunti kumi na tano kuanzia wiki ya kwanza ya Mwezi Desemba.

Kupitia taarifa, Mkurugenzi wa idara hiyo Stella Aura amesema mvua hiyo itakuwa katika ya asilimia 33 na 66.

Mvua ya viwango vya milimita 30 itashuhudiwa kwenye Eneo la Kaskazini na kuongezeka hadi 40 katika maeneo ya Kusini Mashariki, Pwani, Magharibi na Kati.

Maeneo mengine ambayo yatapata mvua kubwa  ni Garissa, Mandera, Marsabit, Nyeri, Isiolo, Kisii, Nyandarua, Laikipia, Kiambu, Murang’a, Embu, Meru na Kirinyaga.

Mvua hiyo pia itanyesha kwenye Kaunti za  Samburu, Bomet, Nakuru, Tharaka Nithi, Baringo, Migori, Nandi, Homa Bay, Kisumu, Busia, Kwale, Kilifi, Tana River, Lamu, Kajiado, Narok, Kitui, Kakamega, Mombasa, Siaya na Nyamira.

Aura amesema mvua hiyo huenda ikisababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi huku wananchi wakitakiwa kuwa macho kuepusha hasara na vifo.