×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Sina chuki na Rais Kenyatta, Jaji Maraga asema

Sina chuki na Rais Kenyatta, Jaji Maraga asema

Jaji Mkuu David Maraga amewahimiza Wakenya kupinga mapendekezo yoyote kupitia Mpango wa Upatanishi BBI yanayolenga kuhujumu uhuru wa Idara ya Mahakama.

Maraga aidha ameendeleza shutma dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta kwa kuhujumu utendakazi wa mahakama akisema licha ya yote hana chuki ya binafsi.

Akizungumza wakati wa hotuba yake ya mwisho, Maraga amesema mapendekezo yanayolenga kugawanya mamlaka ama kuhujumu uhuru wa idara hiyo lazima yapingwe vikali.

Maraga amelenga pendekezo la BBI kutaka Tume ya Utawala wa Haki, Ombudsman kuteuliwa na rais akisema hiyo ni njama ya kutatiza uhuru wa mahakama.

Amesema kufanya hivyo kutarejesha mhakama katika hali ya awali kabla ya kupitishwa kwa katiba ya mwaka wa 2010.

Maraga aidha amemshtumu vikali Kenyatta kwa kutowaidhinisha majaji 41 waliopendekezwa na Tume ya Huduma za Mahakama JSC,  akisema hatua hiyo ni kinyume na sheria.

Maraga amesema rais hana mamlaka ya kupinga au kuuliza maswali kuhusu majaji wanaoteuliwa na JSC