×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mkurugenzi wa DCI akashifiwa na waathiriwa wa ghasia za 2007

Mkurugenzi wa DCI akashifiwa na waathiriwa wa ghasia za 2007

Baadhi ya waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007 wamepuuza tetesi kwamba wanataka kesi za ghasia hizo kufufuliwa.

Watu hao ambao mapema wiki iliyopita walifanya kikao na Mkuu wa Idara ya Upelelezi, DCI George Kinoti wamemshtumu kwa madai ya kuwahadaa kuzungumzia suala hilo.

Waathiriwa hao vilevile wamepuuza madai kwamba maisha yao yamo hatarini huku wakisema wanaishi kwa amani na wenzao.

Aidha, wamesema wanaunga mkono mchakato wa BBI

Jumatano wakati wa Uzinduzi wa Shughuli ya ukusanyaji saini za kufakikisha kura ya maamuzi, Rais Uhuru Kenyatta alikashifu hatua ya DCI kurejelea kesi hizo.