
Mahakama imetupilia mbali ombi la aliyekuwa Mkurugenzi wa Dijitali katika Ikulu Dennis Itumbi kutaka aruhusiwe kuwasilisha kesi dhidi ya Waziri wa Masuala ya Ndani ya nchi, Fred Matiang'i.
Hakimu Douglas Ogoti,amesema Itumbi hakuielezea mahakama jinsi alivyopata taarifa na stakabadhi alizonuia kutumia dhidi ya Matiangi.
Ogoti amesema kwa sababu Itumbi hakuelezea jinsi alivyopata taarifa hizo na stakabadhi haziwezi kutumika.
Miongoni mwa stakabadhi alizowasilisha Itumbi ni barua iliyoandikwa na Wizara ya Fedha , Kamishna wa Ardhi na wizara ya Elimu.
Aidha, Mahakama imesema hana idhini ya kutumia stakabadhi zilizoidhinishwa kuwa za umma, ambazo hazina saini.
Itumbi alitaka kuruhusiwa kuwasilisha kesi dhidi ya Matiangi kwa madai kwamba alihusika katika unyakuzi wa ardhi ya Ruaraka alipokuwa Waziri wa Elimu.