
Kiongozi wa KANU Gidion Moi amepuuza dhana kwamba wakazi wa eneo la Bonde la Ufa wanapinga Mpango wa Upatanishi BBI.
Akizungumza wakati wa kampeni yake ya kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za kutia saini za kufanikisha kura ya maamuzi katika kaunti ya Migori, Moi ambaye pia ni Seneta wa Baringo amesema ana imani kwamba BBI inaungwa mkono na Wakenya wa matabaka mbalimbali.
Amewakashifu viongozi wanaolenga kutumia BBI kuwagawanya wananchi kwa misingi ya kikabila.
Aidha, Moi amesema ataungana na viongozi mbalimbali nchini kuhakikisha BBI inapata uungwaji mkono kwa misingi kwamba itapiga jeki uongozi wa taifa hili.