
Mahakama imemruhusu Agnes Wangui anayejidai kuwa mke wa Marehemu Mbunge wa Matungu, Justus Murunga kufanya uchunguzi wa DNA ili kuthibitisha kwamba Marehemu ndiye baba wa wanawe.
Hakimu wa Mahakama ya Milimani Peter Muholi ameagiza uchunguzi huo kufanyika katika Hifadhi ya Maiti ya Lee.
Aidha, Hakimu Muholi ameruhusu hafla ya mazishi kufanyika akisema familia ndiyo itakayoamua siku ambapo mwili wa marehemu utazikwa.
Aidha Wangui pamoja na wanawawe wawili wameruhusiwa kuhudhuria hafla hiyo pamoja na kushiriki katika mipango ya mazishi.