
Rais wa Marekani, Donald Trump amesema ataondoka Ikulu ya White House iwapo Joe Biden atathibitishwa kuwa rais wa 46 wa taifa hilo na wajumbe wa Congress, japo itakuwa vigumu kukubali matokeo.
Akizungumza na wanahabari, Trump ambaye amekataa kukubali matokeo tangu uchaguzi ulipofanyika Novemba 3 hata hivyo amesema taila la Marekani litakuwa limekosea kwa kumchagua Biden.
Kufikia sasa Biden ana kura 306 za wajumbe hao zilizohesabiwa huku Trumpa akiwa na kura 232.
Ili kuwa rais ni lazima mshindi apate kura zaidi ya 270 za wajumbe wa Congress.
Mapema wiki hii, Trump alikubali kuruhusu kuanza kwa shughuli rasmi ya kumkabidhi Biden mamlaka licha ya awali kupinga matokeo ya uchaguzi na kulazimu kuhesabiwa upya kwa kura.
Iwapo ushindi wa Biden utathibitishwa, ataapishwa rasmi Januari 20 kuchukua hatamu za uongozi