×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mipango ya kuibadili IEBC ingalipo, ODM yasema

Mipango ya kuibadili IEBC ingalipo, ODM yasema

Shinikizo la kuifanyia marekebisho Tume ya Uchaguzi IEBC lingalipo licha ya  kuondolewa kwa pendekezo kwamba vyama vya kisiasa viruhusiwe kuwateua makamishna wa tume hiyo kwenye Ripoti ya BBI.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa ODM, Edwin Sifuna, mabadiliko katika IEBC yanaweza kufanywa kupitia bunge.

Pendekezo hilo liliondolewa kwenye Mswada wa Marekebisho ya Katiba wa 2020 uliozinduliwa Jumatano na rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa Chama hicho cha ODM ambaye alionekana kujikanganya kwa kushinikiza pendekezo hilo ilhali lilikuwa limeondolewa.

Hata hivyo, Raila amejitetea dhidi ya madai kwamba hakuna na ufahamu kuhusu marekebisho kwenye ripoti ya BBI akisema alihusika kikamilifu.