×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

EACC yatakiwa kuwachunguza maafisa kadhaa wa KEMSA

EACC yatakiwa kuwachunguza maafisa kadhaa wa KEMSA

Kamati ya Afya katika Bunge la Kitaifa imeitaka Idara ya Upelelezi, DCI na Tume ya Maadili na Kukabili ufisadi, EACC kuwachungumza maafisa kadhaa wa Mamlaka ya Usambazaji wa Vifaa vya Matibabu, KEMSA kwa kukiuka sheria katika ununuzi wa vifaa vya kulikabili janga la korona.

Katika ripoti iliyowasilishwa bungeni na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Sabina Chege, miongoni mwa wale ambao kamati imependekeza wachunguzwe ni aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa KEMSA, Jonah Manjari, aliyekuwa afisa wa fedha, aliyekuwa afisa wa mauzo vilevile aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi kwa madai ya kuifanya KEMSA kupoteza shilingi bilioni 2.1 kupitia ununuaji wa vifaa vya kukabili korona nje ya bajeti iliyoidhinishwa.

Mapendekezo mengine katika ripoti hiyo ni kuchunguzwa kwa kampuni 83 ambazo zilisambaza vifaa mbalimbali kwa KEMSA kubaini iwapo zilizingatia sheria katika kufanya hivyo ama zilipata tenda kwa njia ya ulaghai. Wakati uo huo, ripoti hiyo imetoa kipindi cha siku 14 kwa KEMSA kuhakikisha inasambaza vifaa vya korona ambavyo viko katika hifadhi zake ili kutumiwa hasa na wahudumu wa afya wanaovihitaji. Joshua Kutuny ni Mwanakamati.

Hata hivyo Mbunge wa Tharaka, George Murugara ameelezea wasiwasi kwamba huenda mapendekezo yaliyoko katika ripoti hiyo yakakosa kutekelezwa. Amesema ingekuwa vyema kwa kamati hiyo ya afya kutoa makataa kwa idara za uchunguzi ya kutekeleza mapendekezo hayo.