
Maelfu ya Raia wa Argenina hivi sasa wanaendelea kumpa heshima zao za mwisho aliyekuwa mchezaji maarufu wa soka Diego Maradona kufutaikifo chake hapo jana. Mwili wa Maradona umelazwa katika mejengo ya Ikulu ya Argentina japo haujawekwa wazi kwa ajili ya kutazamwa.
Hata hivyo raia wamepigga foleni ndefu huku wengine wakiwa wamekesha katika majengo hayo ili angalau kulitazama jeneza lake ambalo limekuwapo tangu usiku.
Diego alieyeaga dunia akiwa na umri wa miaka 60 baada ya kupata mshtuko wa moyo anatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Jardin De Paz ambapo pia wazazi wake wamezikwa