×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Nafahamu kilichoko katika Mswada wa BBI2020-Odinga

Nafahamu kilichoko katika Mswada wa BBI2020-Odinga

Baada ya Kinara wa ODM, Raila Odinga hapo jana kuzungumzia na kutetea uteuzi wa Makamishna wa IEBC kufanya na vyama vya kisiasa ilhali pendekezo hilo halipo katika ripoti ya mwisho ya BBI, ametuma taarifa kwa vyombo vya habari  akijitetea kutokana na madai kwamba huenda hakuwa na ufahamu wa marekebisho yaliyofanyiwa ripoti ya BBI.

Katika taarifa, Msemaji wa Raila, Dennis Onyango amesema Raila ana ufahamu wa mabadiliko yote yaliyofanywa na kwamba alichofanya jana ni kufafanua pendekezo la awali lililozua ubishi vilevile kusisitiza kwamba mapendekezo yote yakiwamo yake yasingejumuishwa. 

Alipozungumza jana, Raila aliusifu uchaguzi mkuu wa mwaka 2002 uliosimamiwa na makamishna zaidi ya ishirini waliochaguliwa na vyama mbalimbali vya kisiasa akisema hali hiyo ilifanikisha uchaguzi huru na wa haki.