×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

27 walazwa hospitalini baada ya kunywa mursik yenye sumu

27 walazwa hospitalini baada ya kunywa mursik yenye sumu

Watu ishirini na saba wakazi wa Eneo Bunge la Mlima Elgon kwenye Kaunti ya Bungoma wanaendelea kutibiwa katika hospitali mbalimbali baada ya kudaiwa kunywa maziwa ya mala yaani Mursik yanayodaiwa kuwa na sumu.

Chifu wa Kata ya Chongeywo, Eliud Kiptaalam amesema wakazi hao wa Kijiji cha Chelebei walianza kukumbwa na maumivu ya tumbo baada ya kuyanywa maziwa hayo waliyoyanunua kutoka kwa mfanyabiashara mmoja siku ya Jumanne.

Kwa upande wake Afisa msimamizi wa Hospitali ya Mungu Ndogo ya Kopsiro, Kiosang Masaai amesema wagonjwa wote waliofikishwa hospitalini humo kutoka eneo la Chelebei wanaendesha na kutapika, akitoa wito kwa wote waliotumia maziwa hayo kufika hospitalini ili wapimwe na kutibiwa.