
Rais Uhuru Kenyatta amelihimiza jeshi la Kenya kuendelea kuwekeza katika mafunzo ili kuendana na changamoto za kisasa za kiusalama.
Akizungumza katika Kituo cha Mafunzo ya Jeshi cha Lanet, Kenyatta amekariri haja ya maafisa wa jeshi kuwa na uwezo wa kukabili changamoto mbalimbali zinazoibuka katika karne ya sasa kupitia mafunzo ya kisasa.
Maafisa waliofuzu ni kundi la nane kupitia mafunzo ya Sayansi ya Masuala ya Jeshi yaliyotolewa kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Kenyatta.
Maafisa mbalimbali pia wametuzwa kwakuibuka bora katika vitengo mbalimbali. Brian Ngure liibuka kuwa bora katika kitengo cha usimamizi huku Denis Melita piakiibuka bora katika masomo ya kitaalam.
Wengine waliotuzwa ni Safia Dida, Paul Odhiambo, David Gitonga, Lopua Elimlim, Mika Mohamed Yona miongoni mwa wengine. Hafla hiyo imehuhduriwa na Waziri wa Ulinzi Monicah Juma na Mkuuwa Majeshi Robert Kibochi miongoni mwa wengine.