×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

780 waambukizwa korona, 10 wafariki

780 waambukizwa korona, 10 wafariki

Kiwango cha maambukizi ya virusi vya korona kimepungua leo hii kwa asilimia 2.1 ambapo ni asilimia 12.6 kulinganisha na asilimia 14.7 ya jana.

Katika taarifa, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema leo hii idadi ya maambukizi imefikia watu elfu themanini, mia moja na wawili baada ya watu wengine mia saba themanini kuambukizwa virusi hivyo.

Haya yanajiri baada ya kupimwa kwa sampuli elfu sita, mia moja hamsini na nane katika saa ishirini na nne zilizopita.

Miongoni mwao, watu mia saba hamsini na wanne ni Wakenya isipokuwa ishirini na sita ambao ni raia wa kigeni. Aidha, mia nne na sitini ni wanaume, wanawake wakiwa mia tatu ishirini. Mtoto wa mwaka mmoja na mkongwe wa miaka tisini na minne ni miongoni mwa walioambukizwa.

Habari njema ni kwamba watu wengine mia tano hamsini na wawili wamepona na kufikisha idadi jumla ya waliopona kuwa watu elfu hamsini na watatu, mia tano ishirini na sita.

Mia nne sitini na wanane walikuwa wakihudumiwa nyumbani, themanini na wanne wakiwa wale waliolazwa katika hospitali mbalimbali.

Hata hivyo, watu kumi wamefariki kufuatia makali ya Covid-19, idadi ya vifo ikifikia elfu moja, mia nne ishirini na saba kote nchini.

Wakati uo huo, watu elfu moja, mia mbili thelathini na wawili wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini. Elfu saba, mia mbili tisini na watano wanahudumiwa nyumbani, hamsini na saba ni wale waliolazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi, thelathini na wawili miongoni mwao wanatumia vipumuzi, ishirini wakitumia oxijeni.

Watu wengine hamsini na wanane wamelazwa katika wadi za jumla, ishirini na wanne wakilazwa katika vyumba vinavyohitaji uangalizi wa karibu.

Share this: