×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

DCI anatumika kufufua kesi kuhusu machafuko ya 2007/8, Jane Kihara

DCI anatumika kufufua kesi kuhusu machafuko ya 2007/8, Jane Kihara

Viongozi mbalimbali wanaendeleza shutma dhidi ya Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi, DCI George Kinoti kufuatia matamshi yake kwamba ataendelea na uchunguzi wa kesi za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.

Viongozi hao wakiwamo , Wabunge, mwakilishi wa kike na Seneta wa Nakuru, wamedai kwamba baadhi ya wanasiasa wanalenga kuitumia ofisi ya DCI kuendeleza siasa zao.

 Wameonya kwamba iwapo kesi hizo zitafufuliwa basi huenda ikaibua mgawanyiko hata zaidi nchini.

Wakizungumza mjini Naivasha wakati wa Mkutano na Tume ya Uwiano na Utangamano NCIC, wamesema kuna haja kwa viongozi kuwa mstari wa mbele kuhubiri amani.

Mbunge wa Naivasha mjini Jane Kihara, amesema baadhi ya wakimbizi wa humu nchini wamefahamishwa na mbunge mmoja maalum kurekodi taarifa kuhusu ghasia hizo.

Amemkosoa Kinoti kwa kukubali kuchukua hatua hiyo kabla ya kufikiria kwanza athari yake.

Mwakilishi wa Kike Liza Chelule amempongeza Rais Uhuru Kenyatta kwa msimamo wake kuhusu taarifa hiyo ya DCI, Kauli ambayo imesisitizwa na Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri ambao wanadai kuna baadhi ya wanasia wanaopanga kuzua uhasama miongoni mwa jamii mbalimbali.

Mwenyekiti wa NCIC Samuel Kobia amesema wanashirikiana na wanasiasa kuhakikisha amani inaendelea kudumishwa nchini.

Haya yanajiri huku Wawakilishi Wadi wa Bunge la Kaunti ya Trans Nzoia wamemrai Rais Uhuru Kenyatta kumfuta kazi Kinoti.
Mwakilishi Wadi wa Kinyoro, Laurance Mokosu amesema mara kadhaa Kinoti amekuwa akizungumzia masuala fulani bila kuwazia athari zake.