×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Shughuli ya kukusanya saini inaendelea nchini

Shughuli ya kukusanya saini inaendelea nchini

Katika kipindi cha wiki moja pekee Kamati ya Kiufundi ya BBI inalenga kukusanya saini milioni moja za kufanikisha mpango wa kuifanyia katiba marekebisho.

Baada ya kuzinduliwa kwa mpango huo hapo jana, Mwenyekiti wa kamati hiyo Junet Mohammed alisema kwamba wanatarajia kukamilisha shughuli hiyo katika kipindi kifupi zaidi alivyosema awali Kiongozi wa ODM Raila Odinga.

Junet amesema ili kuhakikisha Wakenya wengi zaidi wanashiriki,  shughuli hiyo pia inaweza kufanikishwa kupitia Mtandao.

Kulingana na sheria, IEBC inahitaji saini milioni moja pekee lakini kamati hiyo imesema kwamba inalenga kukusanya zaidi ya milioni nne huku wadadisi wa masuala ya kisiasa wakisema kwamba hatua hiyo ni ya kutaka kuonesha kwamba Uhuru na Odinga wana umaarufu mkubwa na kwamba BBI itaungwa mkono na Wakenya wengi zaidi wakati wa kura ya maamuzi iwapo itafanyika.

Hayo yanajiri huku Kenyatta na Odinga wakiendelea kuwarai  Wakenya kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha mchakato huo wa BBI .

Rais ameendelea kusisitiza umuhimu wa mpango huo kwa utangamano wa taifa.Kwa upande wake Odinga amerejelea umuhimu wa shughuli nzima katika kulivusha taifa la Kenya ng'ambo ya pili kimaendeleo na kitaifa.

Raila ameyatetea baadhi ya mapendekezo akisema lengo la BBI ni kuboresha uongozi huku mengine yakifanywa kupitia sera na sheria.