×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wakenya waraiwa kusaini marekebisho ya katiba

Wakenya waraiwa kusaini marekebisho ya katiba

Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa ODM Raila Odinga wamewarai Wakenya kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha mchakato wa BBI kwa kutia saini Mswada wa Marekebisho ya Katiba.

Rais Kenyatta ameanza kwa kukariri umuhimu wa mabadiliko yanayoendana na wakati na haja ya ujasiri wa kuchukua hatua za mageuzi ili kuafikia malengo ya taifa hasa katika kufanikisha uwakilishi sawa wa kijinsia na mfumo wa ugatuzi.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa shughuli hiyo, Raila amerejelea umuhimu wa shughuli nzima katika kulivusha taifa la Kenya ng'ambo ya pili kimaendeleo na kitaifa.

Pia amechukua muda kutetea baadhi ya mapendekezo ambayo yamezua pingamizi.

 

Kuhusu mbinu za kuchagua wanachama wa tume ya uchaguzi Raila amesema mfumo wa vyama kuwachagua wawakilishi umetumika katika mataifa mengi duniani ikizingatiwa kwamba kila mtu huwa na miegemeo.

Hayo yanajiri huku kiti cha Naibu wa Rais William Ruto kikionekana jukwaani licha ya kwamba ratiba ya leo hamworodheshi kuwa miongoni mwa walioalikwa hivyo kuzua maswali iwapo alisusia ama hakualikwa.

Shughuli ya ukusanyaji saini za kufanikisha BBI imeanza mara moja huku Mkenya kwa jina Emily Wanjiku akiwa wa kwanza kusaini ili kufanikisha mchakato wa BBI. Shughuli hiyo imeanza  ikiongozwa na mmoja wa wenyekiti wa kamati ya kiufundi ya kufanikisha BBI Dennis Waweru.

Wakenya hao wameafutiwa na viongozi wa vyama mbalimbali huku wa kwanza akiwa Mwenyekiti wa Chama cha Mashinani Isaac Ruto, Alfred Mutua wa Maendeleo Chap Chap na Gideon Moi wa Chama cha KANU.

Moses Wetangula na Wafula Wamunyinyi wametia saini ka niaba ya FORD Kenya. Wengine katika ordha ya viongozi wa vyama ni Ali Hassan Joho, Charity Ngilu ambaye ni Gavana wa Kitui, Farah Maalim akimwakilisha Kalonzo Musyokawa Wiper, Musalia Mudavadi wa ANC, Wycliff Oparanya miongoni mwa wengine.

Mwenyekiti mwenza wa Kamati ya Kiufundi Junet Mohammed, amesema  Wakenya wanaweza kusaini kupitia mtandao huku pia akielezea mchakato utakaofuatia.