Wawakilishi Wadi wawili wa Bunge la Kaunti ya Nairobi wametakiwa kufika mbele ya Makao Makuu ya Chama cha Jubilee baada ya kukiuka baadhi ya misimamo ya chama hicho.
Wawili hao ambao ni Wawakilishi wadi maalum Ann Thumbi na Silvia Museiya wametakiwa kujiwasilisha mbele ya Kamati ya Nidhamu katika ofisi za Jubilee eneo la Pangani Ijumaa hii saa nne asubuhi.
Miongoni mwa masuala ambayo yanatarajiwa kuibuliwa ni kuhusu kupitishwa kwa Mswada wa Ugavi wa Mapato ya Serikali ya kaunti, mswada ambao ulikataliwa na Gavana Mike Sonko. Wawili hao wamekuwa wakipinga hadharani kupitishwa kwa mswada huo.