
Wamiliki wanne wa ardhi ambazo zilitwaaliwa na serikali kwa lazima ili kufanikisha ujenzi wa Reli ya Kisasa, SGR watalazimika kusubiri zaidi kabla ya kulipwa fidia.
Kucheleweshwa huko kunatokana na agizo la Mahakama ya Rufaa la kutaka mpango huo wa fidia kusitishwa kwa muda. shughuli ambayo ilikuwa ikiongozwa na Tume ya Kitaifa ya Ardhi, NLC.
Majaji wa Mahakama hiyo Asike Mkhandia, Fatuma Sichale na Jamila Mohammed wamesitisha shughuli hiyo ambapo wamiliki hao wangelipwa jumla ya shilingi bilioni moja, hadi wakati kesi waliyowasilisha wakilalamikia kuwachwa nje ya shughuli hiyo itakaposikilizwa na kuamuliwa.