×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mwanamme amuua mkewe baadaya kuzozania shilingi 600

Mwanamme amuua mkewe baadaya kuzozania shilingi 600

Mwanamme mwenye umri wa miaka 60 anazuiliwa na polisi katika Eneo Bunge la Shinyalu, Kakamega kwa tuhuma za kumuuwa mkewe wa miaka 57 kufuatia mzozo wa shilingi 600.

Kulingana na wakazi, mshukiwa Joseph Amulabu alimpiga mkewe kwa silaha butu wakizozania shilingi 600 alizopata baada ya kuuza chang'aa.

Hata hivyo, familia ya marehemu inasema kuwa mshukiwa amekuwa na tabia ya kumpiga mkewe mara kwa mara.

Familia ya mshukiwa inasema kuwa kulingana na mila na tamaduni ya jamii hiyo , hawatamruhusu kurudi kutangamana na familia yake tena.