×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Aliyekuwa Mbunge wa Kilifi Kaskazini Mustaffa Idd aaga dunia

Aliyekuwa Mbunge wa Kilifi Kaskazini Mustaffa Idd aaga dunia

Viongozi mbalimbali wa eneo la Pwani wanaendelea kutuma risala za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Kilifi Kusini Mustafa Idd ambaye amefariki dunia mapema leo.

Kupitia mtandao wake wa Facebook Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa ameomboleza kifo cha Idd ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Usambazaji maji ya Coast Water.

Kwa upande wake Mbunge wa Kilifi Kazkazini Owen Baya amemtaja marehemu kuwa kiongozi shupavu aliyezingatia maslahi ya wakazi bila ubaguzi.

Viongozi wengine ambao pia wametuma risala za rambirambi ni Mbunge wa Kinango Banjamin Tayari na wa Kaloleni Paul Katana.

Mustafa ambaye pia alikuwa mwanachama na mshauri wa Vugu Vugu la Mageuzi ya Pwani anatarajiwa kuzikwa baadae leo hii nyumbani kwake kwenye eneo la Bomani, Kikambala.

Idd alikuwa Mbunge wa Kilifi kusini kati ya mwaka wa elfu mbili kumi na tatu hadi elfu mbili kumi na saba alizaliwa tarehe kumi na moja mwaka wa elfu moja kendamia sabini katika kijiji cha Majajani, Kilifi Kazkazini.

Kabla kuchukua wadhifa huo alikuwa mwanahabari aliyefanyakazi na shirika moja la habari la KBC.