
Mahakama moja ya Nairobi imetoa agizo la kukamatwa kwa Mbunge wa Kimilili, Didmus Baraza ili ahudumu kifungo cha miezi sita jela.
Barasa alikuwa amepewa makataa ya hadi leo na Mahakamaya Milimani kumlipa wakili mmoja shilingi milioni 1.8 baada ya kumwakilisha katika kesi ya kupinga ushindi wake wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.
Hakimu DM Kivuti ametoa agizo hilo baada ya Barasa kukosa kujiwasilisha mahakamani leo hii kwa kikao cha kesi dhidi yake.
Katika vikao vingine saba vya kesi dhidi yake vilivyofanyiksa awali,Mbunge hiyo aliiomba mahakama kumpa muda wa kuzilipa fedha hizo japo hajafanya hivyo kufikia sasa.