×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Upelelezi DCI George Kinoti amebatilisha msimamo wake kuhusu hatua ya kufufua kesi za ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.

Katika taarifa yake kwenye vyombo vya habari, Kinoti amejitetea akisema hatua ya idara yake haimaanishi kuwa faili za kesi zilizosikilizwa na kuamuliwa zitafunguliwam upya kwa uchunguzi na kwamba yanayozingatiwa ni madai mapya ya vitisho kwa waathiriwa wa ghasia hizo.

Uchunguzi huu unajiri miaka saba baada ya serikali kutangaza rasmi kwamba hapakuwa na ushahidi wa kutosha wa kuwafungulia mashtaka waliohusika katika ghasia hizo zilizosababisha vifo vya watu zaidi ya elfu moja mia moja huku wengine elfu mia sita hamsini kuhama kwao.

Aidha unajiri wiki tatu baada ya Wakili Paul Gicheru kujisalimisha katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC jijini The Hague nchini Uholanzi, katika hatua ambayo wengi wanasema huenda ikawa njama ya kufufua kesi inayomkabili Naibu wa Rais William Ruto.

Baada ya kukutana na waathiriwa wa ghasia hizo na kurekodi taarifa sabini na mbili za mauaji, arubaini na nne za watu kuhama kwao vilevile mia moja na kumi na nane za vitisho, Kinoti alitangaza kuanza mara moja kwa uchunguzi na hata kuwataka kuwa tayari kutoa ushahidi mahakamani.

Aliahidi kufanya kila awezalo kisheria kuhakikisha kwamba waliohusika katika ghasia hizo wanakabiliwa vilivyo.