
Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi ametaja hatua ya kufufuliwa kwa kesi za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/08 kama njama za baadhi ya wanasiasa wanaolenga kutatiza azma ya Naibu Rais William Ruto kuliongoza taifa.
Akizungumza na wanahabari nyumbani kwake, Sudi amesema kuwa Mkuu wa Idara ya Upelelezi George Kinoti na maafisa wengine serikalini wanatumiwa kuendeleza mpango huo ambao anadai unalenga kuzua uhasama baina ya jamii zilizozozana wakati huo na kuhujumu amani nchini.
Hata hivyo Sudi amewashauri Wakenya kuendeleza kuishi kwa amani na kutokubali kuchochewa na wanasiasa