×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wizara ya Fedha yashtumiwa kwa kuendelea kuchelewesha fedha za kaunti

Wizara ya Fedha yashtumiwa kwa kuendelea kuchelewesha fedha za kaunti

Wizara ya fedha inaendelea kulaumiwa kufuatia kucheleweshwa kwa shilingi bilioni 78 zilizopaswa kutumwa kwa serikali za kaunti.

Magavana wanasema kwamba hali hiyo imesambaratisha utoaji huduma kwenye kaunti mbalimbali baada ya fedha hizo kucheleweshwa kwa miezi mitatu mfululizo sasa.

Aidha, Kamati ya Uhasibu katika Seneti imewaita wakuu wa idara tofauti katika suala zima la ugatuzi, kujadili changamoto zinazokabili kutolewa kwa fedha hizo.

Miongoni mwa waliotakiwa kufika mbele ya kamati hiyo ni; Waziri wa Fedha Ukuru Yatani, Msimamizi wa Bajeti Margaret Nyakango, Mhasibu Mkuu Nancy Gathungu, Mwenyekiti wa Baraza la Magavana Wycliffe Oparanya, Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi, EACC Twalib Mbarak na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Paul Kariuki.