
Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Fred Matiang'i ameendelea kupigia debe kadi za Huduma Namba akisema kwamba zitachangia pakubwa katika kufanikisha huduma kwa umma.
Akihojiwa na runinga moja ya humu nchini, Matiang'i amesema kwamba iwapo Bunge litaidhinisha utumizi wa kadi hizo, basi huenda zikatumika hata kuwatambua raia sawa na vitambulisho vya sasa. Vilevile, amedokeza kwamba kufikia siku kuu ya Jamhuri mwaka ujao, kila Mkenya atalazimika kuwa na kadi hiyo.
Wakati uo huo, Matiang'i amesema kwamba watazingatia kanuni za Wizara ya Afya wakati wa kutoa kadi hizo kwa umma ikizingatiwa ongezeko la maambukizi ya virusi vya korona.