×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Masomo yamerejelewa kwenye shule kadhaa Nakuru

Masomo yamerejelewa kwenye shule kadhaa Nakuru

Shughuli za masomo zimerejelewa katika shule mbili tofauti kwenye Kaunti ya Nakuru na Taita Taveta baada ya kufungwa kwa wiki mbili kufuatia maambukizi ya korona miongoni mwa wanafunzi na walimu.

Katika Shule ya Upili ya St. Bakhita Bahati, Kaunti ya Nakuru wanafunzi na walimu wamejumuika kufanya maombi ya shukrani baada ya wanafunzi themanini na watatu na walimu watano kuambukizwa virusi hivyo.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mtawa Katherine Wangare amesema wanafunzi na walimu walioathiriwa wanapewa ushauri nasaha.

Wangare amesema kwamba karantini ya wiki mbili imekuwa yenye changamoto nyingi kufuatia hofu miongoni mwa wanafunzi.

Katika Shule ya Msingi ya Voi Taita Taveta, wanafunzi mia tatu thelathini miongoni mwa 350 wa gredi ya nne na darasa la nane vilevile wamerejelea masomo baada ya kujiweka karantini kwa wiki mbili baada ya walimu watatu kuambukizwa korona.

Mwalimu Mkuu, Mumia Mvurya anasema mikakati imewekwa kuhakikisha maambukizi yanakabiliwa shuleni humo.