×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 12 wafariki dunia huku wengine 413 wakiambukizwa korona

Watu 12 wafariki dunia huku wengine 413 wakiambukizwa korona

Watu wengine kumi na wawili wamethibitishwa kufariki dunia kutokana na Covid-19 katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita na sasa kufikisha idadi jumla ya watu waliofariki kuwa elfu moja, mia tatu tisi na wawili.

Aidha kiwango cha maambukizi leo hii ni asilimia 11. 8  ikipungua kwa asilimia 2.8 kulinganishwa na asilimia 14.6 ya jana.

Katika kipindi sawa hicho, watu mia nne kumi na watatu wameambukizwa  virusi vya korona kutokana na sampuli elfu tatu, mia nne themanini na tisa,  hivyo basi kufikisha jumla ya watu elfu sabini na saba, mia saba themanini na watano waliombukizwa nchini.

Miongoni mwa walioambukizwa, mia tatu tisini na tisa ni raia wa Wakenya huku kumi na wanne wakiwa wa mataifa ya kigeni. Mtu mchanga aliyeambukiwa ni wa umri wa miaka mitano na mkongwa tisini na tisa.

Kaunti ya Nairobi inaendelea kuongoza kwa maambukizi mapya ambapo leo watu mia mbili ishirini na tisa wameambukizwa, ikifuatwa na Mombasa arubaini na sita, Kiambu ishirini na wawili, Busia kumi na wanane na Uasin Ngishu kumi na watano.

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, Wizara ya Afya imesema kwamba watu wengine mia tatu tisini na sita wamepona korona, mia tatu ishirini na sita walikuwa wakihudumiwa nyumbani na sabini katika hospitali mbalimbali. Kenya sasa ina jumla ya watu elfu hamsini na mmoja, mia tatu na watatu waliopona.

Jumla ya wagonjwa elfu moja mia moja themanini na wawili wamelazwa kwenye hospitali mbalimbali nchini, elfu saba, mia moja arubaini na wawili wakihudumiwa nyumbani na hamsini na wawili wakiwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Miongoni mwa hamsini na wawili hao, thelathini na wawili wamewekewa vipumizi na kumi na sita oksijeni.

Adha themanini na sita wanaendelea kutumia oxjeni, sabini na wanne wakiwa kwenye wadi mbalimbali na kumi na wawili wakihitaji uangalizi wa karibu.