
Maafisa wa polisi katika kituo cha Webuye kaunti ya Bungoma wanawazuilia vijana 21 wenye umri wa chini ya miaka 18 wakiwemo wasichana 14 na wavulana 7 waliopatikana katika mkahawa mmoja jana jioni baada ya kupata habari kutoka kwa umma.
OCPD wa Bungoma mashariki Valerian Obore amesema kuwa maafisa wa Polisi walivamia mkahawa huo baada ya kuarifiwa na umma kuhusiana na vijana hao wa umri mdogo ambao walikuwa wameingia katika mkahawa huo kusherehekea sherehe ya kuzailiwa ya mmoja wao.
Obore aidha amewataka wazazi kuwa waangalifu na wanao hasa wakti huu wakiwa nyumbani ili kuwaepusha na mambo yasiyofaa ikiwemo unywaji wa pombe