×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Afisa wa Kliniki afariki kutokana na Covid-19

Afisa wa Kliniki afariki kutokana na Covid-19

Afisa wa Kliniki katika Hospitali ya Kajiado amekuwa wa hivi punde kuaga dunia kutokana na ugonjwa wa Covid-19.

Daktari Omar Said ambaye alikuwa mkaazi wa Kibra ameaga dunia katika Hospitali ya Nairobi ambapo amekuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa siku kadhaa sasa. Kwa mujibu wa Daktari Ahmed Khalebi wa Maabara ya LANCET ambaye amemwomboleza kupitia mtandao wa Facebook, Said aliwasiliana naye mapema leo kabla ya kuaga dunia huku kifo chake kikiendelea kudhihirisha hali ngumu ya kikazi wanayopita wahudumu wa afya nchini Kenya.

Muungano wa Maafisa wa Kliniki, KUCO  tayari umetoa makataa ya siku kumi na nne ya mgomo, ukilalamikia  hatua ya serikali kuwatekeleza wakati huu wa korona kwani wengi wao hawana vifaa vya kujikinga, PPEs.

Aidha, wamelalamikia kutolipwa marupurupu yao licha ya kutia saini mkataba wa maelewano. Haya yanajiri siku moja tu baada ya afisa mmoja wa kliniki, Dakta Nira Patel kufariki dunia kutokana na ugonjwa wa Covid-19.

Muungano huo unasema vifo vyote vinavyohusisha wahudumu wa afya vinatokana na kutozingatiwa kwa masharti ya kujilinda dhidi ya virusi hivyo. Vilevile umelalamikia uongozi wa hospitali mbalimbali kutowapa likizo wahudumu wanaogua magonjwa hatarishi.

Peterson Wachira ni Mwenyekiti wa muungano huo akisema iwapo maslahi yao hayatashughulikiwa basi watafanya mgomo na kulemaza shughuli za matibabu.

Haya yanajiri wakati ambapo madaktari chini ya Chama cha KMPDU wakiwa wametangaza mgomo baada ya kukamilika kwa siku 21.

Vilevile madaktari hao wanalalamikia kutolipwa marupurupu, bima ya afya inayoshughulikia magonjwa sugu kama korona miongoni mwa malalamiko mengine.

Ikumbukwe takriban wahudumu wa afya thelathini na wawili wamefariki kutokana na Covid-19.