
Mlinzi mmoja ameuliwa usiku wa kuamkia leo wakati wa tukio la uhalifu katika duka moja kwenye jengo la Mountain Mall kwenye barabara Kuu ya Thika.
Kwa mujibu wa walioshuhudia, mlinzi huyo alivamiwa na washukiwa wa uhalifu waliokuwa wamejihami kwa bastola na wakamuua kwa kumfyetulia risasi kwenye kichwa na kifua.
Washukiwa hao walijidai kuwa wateja katika duka hilo kabla ya tukio hilo huku polisi wakisema kwamba wawili hao walitoweka na begi lililokuwa na kiwango cha pesa ambacho hakijawekwa wazi kufikia sasa.