
Askofu wa Kanisa la Kianglikana Dayosisi ya Kitale, Daktari Emmanuel Chemengich amesema mchakato wa kuifanyia Katiba marekebisho haufai kuzua mgongano wa majukumu wa serikali tendaji yaani The Executive.
Chemengich amesema miongilio ya majukumu huzua mgogoro wa kisheria na kulemeaza upatikanaji wa haki hasa makamani, upasishaji na utiaji saini wa miswada muhimu kuwa sheria na utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini.
Wakati wa kikao na wanahabari katika Kanisa la St Lukes askofu huyo amesema litakuwa jambo la busara maoni ya Wakenya wa matabaka mbalimbali kujumuishwa kuafikia mwafaka kabla kufanywa kwa kura ya maamuzi